Hizi ni baadhi Ya Biashara ambazo hauruhusiwi Kuzitangaza Facebook na Instagram kwa kulipia matangazo (sponsored Ads)...

💘Ikiwa unataka kutangaza Biashara Facebook na Instagram,
Hizi ni baadhi Ya Biashara ambazo hauruhusiwi Kuzitangaza kwa kulipia matangazo (sponsored Ads)...
01. Cryptocurrency
02. Michezo Ya Kubahatisha (kubeti)
03. Silaha za moto - kama vile bunduki, bastola, mabomu, n.k.
04. Sigara na Dawa za kulevya kama vile bangi, cocaine, shisha, n.k.
05. Dangulo (kuuza wanawake au wanaume wa kufanya nao mapenzi)
👎mambo yote ya kingono
06. Huduma za kifedha (kutuma na kupokea pesa).
👉Ni mpaka uwe umeidhinishwa. Hata kama ni kupokea Zaka na Sadaka.
07. Siasa (kufanya kampeni za aina yoyote)
08. Dini (kutangaza dini yako au dhehebu)
09. Huduma na Bidhaa za Afya - ikiwa ni pamoja na kuuza dawa baridi
👉Ndio maana watu wengi wanaouza bidhaa za afya kupitia kampuni za network Marketing (kama vile BF Suma, Nepstar, n.k.) huishia kufungiwa account zao za matangazo (ad accounts).
👉Ni mpaka huduma yako au bidhaa zako ziwe zimeidhinishwa ndipo utakaporuhusiwa kuzitangaza.
10. Vileo (alcohol)
Ni lazima uwe umeidhinishwa kabla ya kuvitangaza.
11. Bidhaa za kupunguza Uzito (weight loss)
Ni lazima uwe umeidhinishwa kabla ya kuzitangaza.
12. Kuwasaidia watu kupata wapenzi (dating services)
Ni lazima uwe umeidhinishwa kwanza hata kama unatumia Aplikesheni, blog, au tovuti (website)
13. Biashara za watu wengine ambazo wenye nazo hawajakuruhusu kuzitangaza
Kwa mfano, kuanza kutangaza Coca-Cola, Pepsi, dstv, n.k.
14. Dawa za Kienyeji na Vitutubisho (supplements)
Ni mpaka uwe umeidhinishwa kwanza (approved).
15. AJIRA (employment)
Kwa mfano, kusema unatafuta mawakala, mfanyakazi wa ndani (House boy au House girl), mlinzi, mhazini, n.k.
16. Real estate (upangaji na uuzaji wa majumba, viwanja, n.k.)
Hapo unatakiwa kupitia sheria zao kwanza na biashara yako kuidhinishwa.
17. Taasisi za elimu - kama vile vyuo.
Hapo unatakiwa kupitia sheria zao kwanza na biashara yako kuidhinishwa.
Kwa Leo tuishie hapo.
Je elimu hii imekusaidia?
Nitafute WhatsApp 0764 793 105 sasa hivi
Kupata mafunzo ya jinsi ya kulipia Matangazo ya biashara yako Facebook kwa kuBoost na kutumia Ads Manager.
Kumbuka, Biashara ni Matangazo (mazuri)
#lacksontungaraza