BIASHARA ( 7 ) ZA KUFANYA MAMA WA NYUMBANI...
February 28, 2023 at 11:25 am
🔥BIASHARA ( 7 ) ZA KUFANYA MAMA WA NYUMBANI
_______________________

Ikiwa u mama wa nyumbani na unatafuta #biashara ya kufanya ili uweze kupatapo FEDHA za kukusaidia katika mambo madogo madogo (ya kwako binafsi na ya familia)...
Basi unaweza kuchagua biashara mojawapo kati ya hizi saba (7) nitakazoziongelea katika mfululilo wa somo hili...
BIASHARA YA KWANZA
"Kuuza Vitafunio/Chakula"
_______________________
👍🏼Mtaji wa kuanzia hii biashara sio mkubwa sana kwa sababu sehemu kubwa ya Vyombo utakavyotumia tayari unavyo nyumbani kwako, au unaweza kuazima kwa #Shosti yako.
👍🏼Na hii ni rahisi; kama huwa unaweza kupikia familia yako na wanakusifia kuwa CHAKULA CHAKO NI KITAMU SANA 😋 basi unaweza kutengeneza PESA NZURI kupitia huo uwezo wako uliojaaliwa na Mwenyezi Mungu 🙏🏼
👍🏼Ila kama bado una mashaka na uwezo wako wa kutengeneza vitafunio (kama vile Maandazi, Chapati, Visheti, Skonzi, n.k) na Chakula... basi unaweza kuingia kwenye mtandao wa YouTube ujifunze. (YouTube kuna video nyingi zinazofundisha BURE).
SASA UNAPATAJE HIZO VIDEO ZA BURE 📹 ?
👍🏼Ingia YouTube, kisha kwenye eneo la kutafuta video za kuangalia (search) andika Jina la video unazotaka kuangalia.
Kwa mfano, kama unataka kujifunza juu ya CHAPATI, unaweza kuandika "Jinsi Ya Kutengeneza Chapati Tamu na Laini"
Utaletewa video nyingi sana... kisha utachagua mwenyewe za kuangalia.
🔥ANGALIZO.
_______________________
1️⃣Mshirikishe #Mumeo kabla ya kuanza ili upate Baraka zake na Sapoti.
Ila hakikisha unatumia mbinu zote kumshawishi mpaka akukubalie 😊
2️⃣Tengeneza Vitafunio/vyakula vinavyopendwa na watu wa hapo unapoenda Kuuza.
Kama wanapenda Chapati, wape Chapati, usiwalazimishe kula Maandazi.
Kwa hiyo, fanya uchunguzi wako kwanza.
3️⃣Kama una kijana #Mwaminifu unaweza kumtumia Kukuuzia mtaani ili wewe uendelee na majukumu yako ya malezi nyumbani.
4️⃣Zingatia UBORA.
Sio leo chakula kinakuwa Kitamu halafu kesho kinakuwa kichungu. WATEJA WATAKUKIMBIA.
5️⃣Hakikisha wateja wako wanajua Ratiba Yako ya biashara.
Wajue unauza lini na lini (siku gani)
Lini hauuzi,
Unauza saa ngapi, na
Unauzia wapi (kama ni nyumbani kwako au sehemu nyingine).
6️⃣Tangaza Biashara Yako kwa majirani zako wote au mtaani.
Biashara ni matangazo.
Bila kutangaza hakuna atakayejua. Na wasipojua biashara yako itakufa kwa kukosa wateja.
Weka aibu pembeni, fanya biashara, wewe ni mwanamke jasiri (super woman 👩).
Pia tangaza kwa watu unaosali nao kanisani au msikitini.
Au wa kwenye vikundi vyenu vya kikabila, VICOBA, n.k.
7️⃣Usile Mtaji wa biashara yako.
Heshimu pesa yako ya biashara.
Hiyo sio pesa ya kwenda kulia bata na kuchangia kwenye shughuli za mashosti zako - kama vile birthday 🎂, kitchen party 🥳, harusi, send-off, n.k.
_______________________
👍🏼Kwa Leo tuishie hapa.
Kesho tutaendelea na biashara ya pili.
Follow hii blog kuendelea kujifunza.
Kama una swali lolote, uliza.
WhatsApp 0764 793 105.

#lacksontungaraza
#superwoman